Thursday, June 27, 2013

HALI YAZIDI KUWA TETE KATIKA CHUO KIKUU CHA TEOFELO KISANJI, UONGOZI WA CHUO NAO WATOA TAMKO .


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari


 Waandishi wa Habari wakiwa nje ya ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo kwa zaidi ya Masaa Matatu
 Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari
 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofelo kisanji wakingoja kusikia Hatima yao


Hali bado ni tete katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha Mgomo huo.
Akisoma Tamko la kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
Hata hivyo Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.

Ameongeza kuwa kama  kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya kubatilisha.

Picha na Mbeya yetu

Thursday, June 20, 2013

SOMA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA JUU YA MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.




 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman
---

MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
--
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE. 

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100. 

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA  
MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.  AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI.

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI.  

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA .

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI .  

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By, 
                           
[DIWANI ATHUMANI  
[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Wednesday, June 19, 2013

LUNDENGA AMTIMUA MISS JUKWAANI BAADA YA KUVAA NUSU UCHI MBELE YA MBUNGE



Mrembo aliyetimuliwa, Saphina Chumba akiwa jukwaani.

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea......

KAULI YA RAIS KIKWETE JUU YA MLIPUKO WA MABOM ARUSHA

Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya Juni 15, 2013, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa....

Tuesday, June 18, 2013

BREAKING NEWZ SAIDA KAROLI AJAFA KAMA INAVO VUMA


Leo kumekuwepo na taarifa kupitia kundi pepe la majadiliano la Mabadiliko-Tanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za asili Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia leo hii katika ajali ya kuzama kwa boti.
Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.
Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”



BOMU ARUSHA... NJAMA NZITO


Na Joseph Ngilisho, Arusha

NYUMA ya matukio ya kigaidi ambayo yamefululiza kutokea jijini Arusha kuna njama nzito baada ya kuibuka maswali mengi yanayosababisha mahali hapa kutokuwa shwari na salama kufuatia bomu lililolipuliwa Jumamosi iliyopita, Uwazi lina uchambuzi....

SIRI NZITO YA KIFO CHA LANGA


Na Mwandishi Wetu
MWILI wa mwanamuziki Langa Kileo jana (Jumatatu) ulipumzishwa kwenye nyumba ya milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar lakini nyuma ya kifo chake kuna siri ambayo rafiki yake wa karibu (jina linahifadhiwa) mkazi wa Mikocheni A jijini Dar ameamua kuiweka hadharani.....