Thursday, June 13, 2013

TAMASHA LA FILAMU GRAND MALT KUFANYIKA MWANZA


Msaani Jacline Walper) wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kufanyika kwa tamasha la filamu jijini  Mwanza kwenye viwanja vya Sahara  ambalo limedhaminiwa na GrandMalt na Isamilo Lodge ya Mwanza...
Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ mwaka huu ambalo linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza.Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo,Mussa Kisoky na kulia ni Meneja Habari na Mahusiano wa TBL,Edith Mushi.
Mratibu wa Tamasha Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’,Mussa Kisoky akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna alivyojiandaa na Tamasha hilo ambalo Mwaka huu litafanyika jijini Mwanza.
Msanii wa Filamu kutoka Bongo Movie,Jacob Steven (kati) akizungumza na vyombo vya habari juu ya Tamasha hilo huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi.
Msanii wa Filamu nchini kutoka Bongo Movie,Jacqueline Wolper akizungumza na vyombo vya habari juu ya Tamasha hilo huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi.
 
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo.
 ****  *****
Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Wazi la Filamu Tanzania maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ mwaka huu linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, wanaamini litafanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mikakati waliyoiweka.
Consolata alisema, tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja hivyo kuanzia Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazoonyeshwa katika kipindi hicho.
 
“Tumejipanga kufanya uhamasishaji wa kutosha ili kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuweza kuhudhuria tamasha hili. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
 
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi alisema kwa ushirikiano na kampuni ya Sophia Records, ambao ndio waandaaji na waasisi wa tamasha hilo, wanaamini litafana na kufanikiwa zaidi mwaka huu.
 
“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana,” alisema.
Edith alisema waliingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini tamasha hilo na kwa sasa wanalipeleka mikoa mingine kama walivyofanya kwa kulipeleka Mwanza kutoka Tanga lilikofanyika mwaka jana.
 
“Tunawaahidi Watanzania wote kwa ujumla, kuwa tamasha hili litakuwa na mvuto wa aina yake na hatimae kutumika kulitangaza Taifa letu kupitia tasnia hii ya filamu ambayo kwa sasa inakua kwa kasi kubwa,” alisema Edith na kutaka kampuni au taasisi nyingine kujitokeza ili kuwa wadhamini wenza.
 
Naye Mkurugenzi wa Sophia Records walio waandaaji na waasisi wa tamasha hilo, Musa Kissoky alitoa shukrani kwa Grand Malt kulidhamini hivyo kuliboresha kwa kiasi kikubwa.
“Tunawashukuru sana Grand Malt na wasanii wa Bongo Movie, hususan uongozi wao, kwa ushirikiana mkubwa wanaotupatia katika kuhakikisha tamasha hili linafanikiwa.”
Tamasha hilo litakuwa likianza asubuhi hadi usiku na kutakuwepo na burudaniu mbalimbali zitakazosindikiza na hakutakuwa na kiingilio, huku akisema bendi ya Extra Bongo watakuwepo siku ya uzinduzi.
 
Wasanii wote maarufu wa filamu wanatarajia kutua Mwanza Juni 29, ambapo siku hiyo watajumuika na wakazi wa Mwanza ndani ya Club Lips na siku inayofuata watashiriki katika shughuli za kijamii katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure, ambapo watatoa vyandarua zaidi ya 1000.
 
Akizungumzia tamasha hilo, mwigizaji Jacqueline Wiolper alisema, wana furaha kubwa na wanaamini watapata mengi zaidi wakati wote wa tamasha hilo.
Tamasha hilo linadhaminiwa kwa mwaka wa tatu sasa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment