Thursday, June 27, 2013

HALI YAZIDI KUWA TETE KATIKA CHUO KIKUU CHA TEOFELO KISANJI, UONGOZI WA CHUO NAO WATOA TAMKO .


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari


 Waandishi wa Habari wakiwa nje ya ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo kwa zaidi ya Masaa Matatu
 Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari
 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofelo kisanji wakingoja kusikia Hatima yao


Hali bado ni tete katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha Mgomo huo.
Akisoma Tamko la kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
Hata hivyo Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.

Ameongeza kuwa kama  kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya kubatilisha.

Picha na Mbeya yetu

Thursday, June 20, 2013

SOMA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA JUU YA MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.




 Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman
---

MAUAJI YA MTU MMOJA KUFUATIA VURUGU YA WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMBILA WILAYA YA MBOZI KUWASHAMBULIA ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA OPERESHENI.
--
MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE. 

CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150 WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA  AINA YA DIESEL MADUMU ZAIDI YA 100. 

HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA  
MADUMU NANE LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.  AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES  S/O JOSE  MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI KITU GANI KILICHOMJERUHI.

PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARANI.  

HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA .

ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI MMOJA  AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI .  

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA HATUA ZINAZOSTAHILI.


Signed By, 
                           
[DIWANI ATHUMANI  
[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Wednesday, June 19, 2013

LUNDENGA AMTIMUA MISS JUKWAANI BAADA YA KUVAA NUSU UCHI MBELE YA MBUNGE



Mrembo aliyetimuliwa, Saphina Chumba akiwa jukwaani.

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea......

KAULI YA RAIS KIKWETE JUU YA MLIPUKO WA MABOM ARUSHA

Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya Juni 15, 2013, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa....

Tuesday, June 18, 2013

BREAKING NEWZ SAIDA KAROLI AJAFA KAMA INAVO VUMA


Leo kumekuwepo na taarifa kupitia kundi pepe la majadiliano la Mabadiliko-Tanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za asili Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia leo hii katika ajali ya kuzama kwa boti.
Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.
Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”



BOMU ARUSHA... NJAMA NZITO


Na Joseph Ngilisho, Arusha

NYUMA ya matukio ya kigaidi ambayo yamefululiza kutokea jijini Arusha kuna njama nzito baada ya kuibuka maswali mengi yanayosababisha mahali hapa kutokuwa shwari na salama kufuatia bomu lililolipuliwa Jumamosi iliyopita, Uwazi lina uchambuzi....

SIRI NZITO YA KIFO CHA LANGA


Na Mwandishi Wetu
MWILI wa mwanamuziki Langa Kileo jana (Jumatatu) ulipumzishwa kwenye nyumba ya milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar lakini nyuma ya kifo chake kuna siri ambayo rafiki yake wa karibu (jina linahifadhiwa) mkazi wa Mikocheni A jijini Dar ameamua kuiweka hadharani.....

HATIMAE JANA RAPPER LANGA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI


Watanzania wakiuaga mwili wa marehem Rapper Langa  nyumbani kwao  Mikocheni, jijini Dar natayari  ameshazikwa katika makaburi ya Kinondoni  saa 10 jioni

Thursday, June 13, 2013

HUYU NDIYE MAMA ALIYEKAA JUU YA PAA KUPINGA NYUMBA YAKE KUUZWA NA BENKI. SHUHUDIA


Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.....

TAMASHA LA FILAMU GRAND MALT KUFANYIKA MWANZA


Msaani Jacline Walper) wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kufanyika kwa tamasha la filamu jijini  Mwanza kwenye viwanja vya Sahara  ambalo limedhaminiwa na GrandMalt na Isamilo Lodge ya Mwanza...

ULEVI NOUMER: KWAKUWA FRIDGE JEUPE AKAJUA CHOO TEH TEHTEH!!!!



Teh teh teh!!!!!!! HEBU CHEKI HII VIDEO YA WIMBO WA "KINDERGARTEN"



Ukiangalia video hii yenye vituko na maneno yanayochekesha sana ikiwashirikisha Robyn, Diddy na Paul Rudd, unaweza kukumbuka ilikuwa vipi kuwa kindergaten, tena kama haujakuwa distructed na kucheka sana kwa ukatuni uliyomo kwenye video hiyo.
ningeweza kujaribu kukuambia nini kimetokea pale  Robyn alipowashawishi

ISHU YA TUZO: SITAKI KUBISHANA NA MSANII YOYOTE WANANJAA "NEY WA MITEGO"



Rapper Ney wa Mitego, kupitia wimbo wa "Nasema nao" alifanikiwa kupata tuzo ya wimbo bora wa hiphop, ambao umesababisha malalamiko kwa baadhi ya wasanii wengine ambao wnaona hakustahili kuchukua tuzo hiyo kwa wimbo huo, huku wengine wakidai Fid q anastahili na wengine kudai Stamina ndio anastahili....leo hii Ney mwenyewe kafunga juu ya swala hilo
"aah wasanii ndio wanaolalamika na wameandika kwenye mitandao, lakini mwisho wa siku lazima tukubali matokeo kwamba mziki unabadilika kila kukicha, mi nawaambia wasanii wenzangu kwamba mkiendelea kung'ang'ania huko mtakufa njaa, halafu mwisho wa siku wataendelea kulia tu kila siku kwamba kuna hili mara lile,mi naimani kwamba mashabiki wangu ndio wamenikabidhi tuzo, media zinazosapoti kazi yangu ndio zimenisaidia mpaka mimi nimezungumza na mshabiki wangu popote walipo mpaka juzi nimepata tuzo ya wimbo bora wa hiphop. mi nastahili kupata tuzo, kwasababu kwanza sijui wao wanafanya hiphop gani, wakae waeleze mziki wao wao ni hiphop kwasababu hii na hii na hii na wangu sio hio hiphop kwasababu hii na hii na hii. bwana hiphop ni ukweli na unabadilika kila siku kila kukicha. Mi nawashauri tu kitu kimoja, sitaki kubishana na msanii yoyote, wana njaa, wakiendelea kung'ang'ania huko watakufa njaa, kwanini watu wamemsapoti Ney, kwanini watu wamemsapoti Kala Jeremiah,angalia mashairi ya Kala yako wazi, lakini we unaweka sijui mafumbo ya dizaini gani nani atakuelewa...........
halafu tuzo sio lazima upate tuzo, sio lazima ulaumu, kuna wasanii wakali hawajawahi kupata tuzo lakini hawajawahi kulalamika, kuna wasanii kama Juma Nature, nani anaweza kusimama stage na Nature? sijawahi kumsikia anaongea.....
category moja tu nimewekwa nimetusua wao wanalia, shauri yenu shauri yenu, jipangeni mwakani, mi staki kubishana nao, am the best, halafu wasipoangalia nawatengenezea kiwanda kwa ajili ya kuwaajiri wanapoendelea kuwana na hali ngumu, natengeneza kiwanda ambacho ntawaajiri wasanii  wanaofeli wote kwasababu hawana shughuli za kufanya." amesea Ney.

MSANII BORA WA HIPHOP ATANGAZA KUGAWA TUZO YAKE KWA MAREHEM ALBERT MANGWEA


Leo hii nimepita ukurasa wamsanii bora wa hiphop, mtunzi bora na aliechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, Kala Jeremiah, na kukutana na ujumbe aliouandika akitangaza kutoa tuzo moja kwa marehem Albert Mangweha a.k.a Ngwea na kuikabidhi kwa mama mzazi wa marehem Albert Mangwea.

''tAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.

mIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.

NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.

TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO

TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.''

POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP.

RAPPER LANGA KILEO A,K,A LANGA AFARIKI DUNIA


Msanii wa hiphop Tanzania, Langa Kileo a.k.a Langa amefariki dunia leo (13th) muda mfupi uliopita  katika hospitali ya muhimbili jijini Dar.Akizungmza na Clouds Fm, Afisa uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Ameniel Aligaesha,

Tuesday, June 11, 2013

POLISI WA KITUO CHA MAGOMENI ATIMULIWA KAZI BAADA YA KUPIGA PICHA ZA NUSU UCHI


POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi  kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni..

HUYU NDIO BABA MZAZI WA WEMA SEPETU

Leo hii kupitia mtandao wa Instagram, Pttiman alitupia picha akiwa baba yake mzazi, mzee Sepetu, huku pembeni akiwepo mtu wake wa karibu sana "Pettiman. Nimeona ni vizuri kushare na wewe, kwasababu nilikuwa sijawahi kabisa kumuona sehem yoyote

MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA


Msanii wa filamu Tanzania Jaji Khamis anaejulikana kama Kashi, amefariki leo hii, akiwa hospitali ya taifa ya Muhimbili, huku kilichomuua hakijajulikana mpaka dakika hii, ila inasemekana alikua anaumwa kiasi cha kushindwa kuongea usiku wa kuamkia jana.
kupitia mtandao wa instagram muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) aliandika 

Ehhh Mungu wangu!!! mona tinaisha hv jamani??? REST IN PEACE DADA CASHY.....uwiii tumrudieni MUNGU jamani...hakuna anejua siku wala saa.

Wema Sepetu nae aliandika 

Inna lillahi wa innah illahi rajoon.....dah tunapukutika tu wallahi...dah

Sunday, June 9, 2013

MISS MBEYA KAPATIKANA JANA TAREHE 8


                              Jana Tarehe nane Ndani ya ukumbi wa City Pub Mbeya .
                                                      Top Five ya Miss Mbeya......

Saturday, June 8, 2013

YALIYO JILI JANA BUB'S LONGUE

Mkulugenzi wa 2sister akiwa anapanga Vinywaji cha Redd's Jana Bubs Loungue

MAANDALIZI YA MISS MBEYA YANAENDELEA.

Bob junior Amewasili mbeya Mida ya saa 8:32 Mchana kutoka Air port ya Songwe
 Mwana habari wa Bomba Fm Chriss Wakimkalibisha Bob junior kwenye open space
ya City Pub Mbeya.
 Maandalizi ya Miss Mbeya ndo yanaendelea.

Thursday, June 6, 2013

MISS MBEYA ITAKAYO FANYIKA TAREHE 8 MBEYA CITY PUB MAANDALIZI YAKE YAMEKUWA YA KUSISIMUA.

 Manager wa Radio Bomba FM Katikati akiwa na Mkulugenzi wa kampuni ya Native Film.
Mrembo akiojiwa na waandishi wa Habari Kutoka ITV na TBC Tv.
Mrembo Aisha Beneke na Sara Samwel wakiwa kwenye picha ya pamoja

Mary Kagali Miss Mbeya 2009 Akiwapa mbinu Warembo alipo watembelea kambini kwenye mazoezi
leo Mtenda Hotel iliopo Soweto Mbeya

MAZISHI YA NGWEA YAKAMILIKA MENEO YA KIHONDA MKOANI MOOGORO


 Hatimae leo hii, msanii Albert Mangwea, amefikishwa katika nyumba yake ya milele, katika makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro, pembeni ya kaburi alilozikwa marehem baba yaje mzazi

MR NICE ATEMWA GRANDPA RECORDS AZIKOSA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 141


 


Baada ya story nyingi kutapakaa, kupitia mitandao mbali mbali hasa ya nchini Kenya, kuwa msanii Mr Nice ametemwa na record iliyokuwa ikimsimamia kazi zake (Grandpa Recods) iliyoko jijini Nairobi kwa kisa cha

Wednesday, June 5, 2013

WANANCHI WA MIKESE WAUSIMAMISHA MSAFARA KUMUAGA NGWEA













Wanamchi wa maeneo ya mikese, wamekusanyika na kuusimamisha msafara uliobeba mwili wa marehem Ngwea kwa kutaka na wao wamuage, akizungumza na Cloud Fm "Moe Fire" amesema walikutana na kundi la watu na kudhani labda kuna tatizo. Baada ya kusimamishwa na trafic na kuuliza tatizo ni nini, Trafic alisema kuwa wananchi hao wamekusanyika na ili kuuaga mwili wa marehem Ngwea na kudai kitendo hicho kikifanyika ndio amani itapatikana.
Kilichofanyika ni kuruhusu watu wle walishike gari lililokuwa na mwili wa Ngwea na kuondoka, lakini baada ya kuondoka, zaidi ya pikipiki 50 walizozikuta pale ziliongoza msafara huku magari mengine pia yakiunga msafara huo. 

MAANDALIZI YA MISS MBEYA YAME PAMBA MOTO.

Baadhi ya Matukio yanayo endelea  Kwenye kambi  la Miss MBEYA mjini 
Mtenda Hotel iliyopo Soweto Mbeya
Baadhi ya kamati ya Maandalizi ya Miss MBEYA  Inayo talaraji kufanyika Tarehe
 nane Mwezi huu.

Huyu ndiye anae kaa na Washiliki wa Miss MBEYA Mjini  Kambini ....